
Staa wa muziki kutoka nchini Tanzania, Raynvanny amehisiwa kuwa huwenda akashiriki ziara ya kimataifa ya nyota wa muziki wa nchini Colombia, Maluma.
Rayvanny anahisiwa kuwa atashiriki ziara hiyo iliyopewa jina la album ya tano ya Maluma ‘Papi Juancho’ inayotarajiwa kuanza rasnu Februari 2021.
Hii ni baada ya ujumbe wa Rayvanny kupitia ukurasa wake wa Instagram Disemba 14 2021 uliosomeka “SIJISIFII TOKA TUPATE UHURU HAUJAWAHI TOKEA WIMBO KAMA HUU EAST AFRICA PERIOD KAMA UNABISHA SEMA WEWE UPI ???
#MAMATETEMA GLOBAL WAY #CHUI @rayvanny @maluma MEET ME ON #PAPIJUANCHO TOUR
ZOMBIE BABA @s2kizzy
Maluma ameshatoa ratiba rasmi ya ziara hiyo ambapo itaanzia Zagreb Croatia, Februrari 24 na kumalizia April 10 huko Tel Aviv nchini Israel.
Hii inafuata baada Rayvanny kuvunja rekodi ya kuwa Msanii wa kwanza kutokea Afrika kutoa burudani kwenye jukwaa la MTV EMA kwa mwaka 2021.
Burudani hiyo ya kihistoria kwa tasnia ya muziki kwa msanii kutoka Afrika akiwakilisha Tanzania ilitolewa kwa wimbo wa Maluma,Mama tetema