
Msanii wa Bongofleva Harmonize na Otile Brown wameingia location kuitayarisha video ya wimbo wao ambao unahisiwa huenda ukapatikana kwenye EP yao ya pamoja.
Harmonize amethibitisha hilo kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram kwa kushare misururu ya picha wakiwa chimbo na mkali huyo kutoka Kenya jambo ambalo limewaaminisha mashabiki muziki mzuri Afrika Mashariki kuwa wawili hao wapo kwenye maandalizi ya video ya wimbo wa pamoja.
Kupitia post hiyo Harmonize hajaweka wazi nini hasa wanapika na Otile Brown ila wajuzi wa mambo kwenye mitandao ya kijamii wanahoji huenda Otile Brown akawa mmoja wa wasanii atakaotumbuiza Disemba 31 mwaka huu kwenye listening party ya album yake ya High Schoolhuko Palm Village, Mikocheni, Dar e Salaam.
Juzi kati Otile Brown alisifia uwezo wa Harmonize katika verse ya wimbo wao wa pamoja waliofanya kwa mara ya kwanza ambapo alisema msanii huyo wa Bongofleva alifanya vizuri katika ngoma hiyo huku akieleza fahari yake kwa mashabiki wa Tanzania na Kenya ambao watakuwa tayari kusikia kazi hiyo
Itakumbukwa Harmonize akiwa nchini katika ziara yake ya kimuziki alitangaza wazi kuja na ‘EP’ itakayo kuwa na nyimbo 5 za pamoja kati yake na Otile Brown.