
Habari nzuri kwa mashabiki wa muziki nchini ni kwamba tutarajie muda wowote ujio wa Collabo kati ya mwanamuziki KRG The Don na Star wa muziki wa dancehall duniani Konshens.
Kupitia insta story ya KRG The Don kwenye mtandao wa Instagram ameshare taarifa hiyo nzuri kwa mashabiki na wadau wa muziki nchini kwa kuthibitisha kuwa tayari wawili hao wamefanya kazi ya pamoja.
Endapo collabo hiyo itatoka itamfanya KRG The Don kuwa msanii wa pili nchini baada ya Ethic Entertainment kufanya kazi ya pamoja na mwanamuziki huyo nyota kutoka Jamaica.
Itakumbukwa kwenye mkesha wa kuamkia mwaka mpya 2022 Konshens alipiga shoo ya kufa mtu kwenye onesho la NRG Wave Concert, shoo ambayo iliyoaacha wapenzi wa muziki mzuri wa dancehall wakitaka burudani zaidi kutoka mkali huyo