
Mwanamitandao aliyegeukia muziki nchini Diana Bahati amemtambulisha msanii wake mpya wake mpya anayekwenda kwa jina la Vinny fleva.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Diana B amesema vinny flava atakuwa chini ya lebo yake ya muziki ya Diana B Entertainment ambayo itasimamia kazi zake zote za muziki huku akiwataka mashabiki zake wamkaribishe msanii huyo ambayo kwa mujibu wake anakuja kubadilisha tasnia ya muziki nchini Kenya.
Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kutofauti kimawazo na diana b ambapo wengi wamehoji amemuiga staa wa muziki nchini Nadia Mukami ambaye juzi kati alimtambulisha msanii wake aitwaye Latinoh chini lebo yake ya Sevens Hub Creative.
Tayari Diana B ameachia wimbo wake mpya uitwao “Mubaba” ambao amemshirikisha msanii wake vinny fleva. Wimbo huo ni watatu kwa Diana B tangu aanze career yake ya muziki baada ya one day na Tuachana tu ambazo aliziachia mwishoni mwaka wa 2021.