Entertainment

DAVID LUTALO AIPIGA CHINI SHOW YAKE YA PASAKA KISA BEBE COOL NA JOSE CHAMELEONE

DAVID LUTALO AIPIGA CHINI SHOW YAKE YA PASAKA KISA BEBE COOL NA JOSE CHAMELEONE

 Nyota wa muziki nchini Uganda David Lutalo amegonga vichwa vya habari nchini humo mara baada ya kufuta performance yake ya Siku Kuu ya Pasaka huko Freedom City..

Kupitia mitandao yake ya kijamii David Lutalo ameandika ujumbe wa kuwaomba radhi mashaiki zake kwa hatua ya kujiondoa kwenye tamasha hilo kutokana na mambo ambayo yapo nje ya uwezo wake.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “In Love” amewashukuru mashabiki kwa ushirikiano na upendo wao huku akiwataka waendelee kumfuatilia kwani ataanika mkeka wa shows zake hivi karibuni.

Hata hivyo David Lutalo hajaweka wazi kilichompelekea kuchukua maamuzi ya kujiondoa kwenye tamasha hilo la siku ya pasaka ila wajuzi wa mambo wanadai kwamba waandaji wa tamasha hilo wameshindwa kuafikia vigezo vya msanii huyo kutumbuiza kwenye show hiyo upande wa malipo.

Ikumbukwe David Lutalo alitarajiwa kushare steji moja na wasanii kama Bebe Cool pamoja na Jose Chameleone.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *