
Mwanamuziki wa nyimbo za injili nchini Size 8 amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya Ringtone kudai kuwa alifukuzwa kwenye uzinduzi wa album yake wikiendi iliyopita.
Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Size 8 amesema amemsamehe ringtone kwa kitendo cha kuvuruga shughuli ya uzinduzi wa album yake huku akipuzilia mbali madai ya kumfukuza msanii huyo kwenye hafla ya kuibariki album yake hiyo kwa kusema kwamba haikuwa kiki kama inavyotafsiriwa kwenye mitandao ya kijamii.
Hata hivyo Ringtone kupitia mitandao yake ya kijamii amesisitiza kuwa Size 8 ni mnafiki na mubaguzi kwenye shughuli zake na kitendo chake cha kumfukuza kwenye uzinduzi wa album yake inaonyesha ni jinsi gani size 8 anawadharau wasanii wa nyimbo za injili.