
Rapa kutoka Marekani DaBaby ambaye yupo midomoni mwa watu baada ya kuenea kwa taarifa zake kuwa alishtakiwa kwa kosa la jinai baada ya Gary Prager, meneja wa mali, kumshutumu yeye na timu yake kwa kumshambulia na kumng’oa jino mwaka wa 2020.
Kufuatia kuenea kwa kasi kwa taarifa hizo hatimaye rappa DaBaby amejibu kwa mara ya kwanza kuhusu madai hayo.
Kupitia video aliyopost kwenye ukurasa wake wa instagram, DaBaby ameonekana kukarisirishwa na kitendo cha kusambazwa kwa taarifa hizo ambazo amedai kuwa ni za uongo licha ya kufikishwa kwenye mamlaka za usalama nchini humo.
Utakummbuka Mwaka wa 2020 iliripotiwa kwamba dababy alikodisha nyumba kwa ajili ya kufanya video, na walikubaliana na mwenye nyumba kuingiza watu 12 tu ndani kulingana na kanuni za COVID-19.
Kinyume na masharti, DaBaby aliingiza watu takribani 40, mwenye nyumba hiyo Gary Pagar alipoamua kumfuata kwa kuvunja masharti ya mkataba, mtu mmoja kutoka kambi ya DaBaby alimvamia na kumuangusha chini.
Baada ya hapo DaBaby alitoka kwenye gari na kumkimbiza pagar hadi ndani nyumba ambapo alianza kwa kumuonya kutowapa taarifa polisi kisha alimtwanga mangumi ya uso hadi kumng’oa jino.