Entertainment

NYOTA NDOGO AFUNGUKA SABABU ZA UKIMYA WAKE KWENYE MUZIKI

NYOTA NDOGO AFUNGUKA SABABU ZA UKIMYA WAKE KWENYE MUZIKI

Msanii mkongwe kwenye muziki, Nyota Ndogo ameweka wazi kwamba kwa sasa hana uwezo wa kutayarisha muziki mpya licha ya mashabiki wengi kumshawishi sana arudi studioni.

Nyota Ndogo amebainisha kuwa kwa sasa anasimamamia Hoteli yake huku akiwasihi mashabiki wake kupromoti biashara yake hiyo.

“Naona mashabiki wanasema nitoe nyimbo sasa mwenyewe nilisahau kuimba, njooni hotelini kwangu munipromoti chakula napika vizuri sana,” Nyota Ndogo ameandika kupitia Instagram.

Mwanamuziki huyo kutoka eneo la Pwani amedokeza kuwa ana mpango wa kufanya media tour hivi karibuni huku akitoa ombi kwa vyombo vya habari kutomhoji kwa Kiingereza kwani hana uwezo wa kuzungumza lugha hiyo kwa ufasaha.

“I was thinking nifanye media tour lakini naomba kuojiwa kwa kingereza tu. Uwa nakiongea vizuri kimoyo moyo lakini nikifungua mdogo balaa.but the more nakiongea nikama mazoezi vile imagine umefungua radio nyota anaongea kingereza simtakufa na vicheko but me I don’t care nitakazana”, Amefichua hilo kupitia Instagram.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *