
Msanii wa Sailors gang,Cocos Juma amedai kwamba wanajuta kujiunga na lebo ya muziki ya Black Market Records.
Katika mahojiano na Plug TV Cocos Juma amekiri kutopata chochote kwenye muziki wao ikiwemo kutomiliki kazi zao za muziki ambazo wamezifanya kwa kipindi chote ambacho amekuwa chini ya lebo ya muziki ya black market records.
Msanii huyo ameenda mbali zaidi na kusema kwamba lebo hiyo inatumia wasanii kujipatia pesa huku ikiwaacha wakiishi maisha ya uchochole.
Hata hivyo ametoa changamoto kwa serikali kuweka mikakati ya kuwalinda wasanii kutoka kwa matapeli kwani vijana wengi wamejipata wakitumia mihadarati baada ya kuporwa mamilioni ya pesa kupitia kazi zao za muziki.
Ikumbukwe wasanii wa Sailors Gang waliingia mkataba na lebo ya muziki ya Black Market Records baada ya kuachana na aliyekuwa meneja wao mwalimu Rachael na tangu wakati huo wamepotea kimuziki.