
Meneja wa Spice Diana, Roger Lubega amemjibu Gravity Omutujju kuonekana kumshambulia katika siku za hivi karibuni kwa kudai kwamba ni mnafiki na hajawahi watakiwa wasanii wengine mema kwenye muziki wao.
Katika mahojiano yake Roger Lubega amesema hana ugomvi wowote na Omutujju huku akidai kuwa rapa huyo anatumia jina la msanii wake Spice Diana kutengeneza matukio ya kuzungumziwa mtandaoni kama njia ya kuitangaza tamasha lake litakalofanyika Cricket Oval Lugogo, Oktoba mosi mwaka huu.
Kwa upande rapa Gravity Omutujju amepuzilia mbali madai ya lubega kwa kusema kwamba mambo yote aliyozungumza juu meneja huyo ni ya kweli huku akisema kwamba hawezi kutumia jina lake kutafuta kiki kwa kuwa yeye ni msanii mkubwa.
Hata hivyo amesema amefanya matamasha makubwa ambayo yamepata mapokezi mazuri kutoka kwa mashabiki bila kutumia kiki huku akitishia kusitisha tamasha lake iwapo watu wataendelea kudai kwamba anatengeza matukio kwa ajili ya kutangaza tamasha hilo.
Utakumbuka mwaka wa 2019 Gravity Omutujju aliwadanganya mashabiki zake kuwa alipigwa risasi tumboni lakini ilikuja ikabainika alitumia njia hiyo kwa ajili ya kutangaza show yake aliyoifanya katika ukumbi wa Cricket Oval Lugogo, nchini Uganda.