Entertainment

DADDY ANDREA NA ANGELLA KATATUMBA WAFUFUA TENA PENZI LAO

DADDY ANDREA NA ANGELLA KATATUMBA WAFUFUA TENA PENZI LAO
Wasanii Angella Katatumba na Daddy Andrea walivunja uhusiano wao mwaka wa 2020 baada andrea kudinda kufanya vipimo vya HIV.
 
Kwenye mahojiano mbali mbali Daddy Andrea alithibitisha kwamba hajawahi mpenda Angella Katatumba na jambo hilo lilimsumbua sana mrembo huyo.
 
Andrea alienda mbali zaidi na kuanza mahusiano mapya na Nina Roz ila mahusiano yao yalikuja yakiingiwa na ukungu kwa madai ya usaliti na kumvunjiana heshima.
 
Sasa mapya yameibuka  baada ya Angella Katatumba kuthibitisha kwamba wamerudiana na Daddy Andrea kwenye moja ya interview.
 
Hitmaker huyo wa amesema amerudiana na mpenzi wake wa zamani Daddy Andrea baada ya prodyuza huyo kumuomba msamaha.
 
Wawili hao wamedai kwamba tayari wamerekodi wimbo wa pamoja uitwao Wendi ambao utatoka hivi karibuni.
 
Ikumbukwe daddy andrea na Angella Katatumba wapo chini ya lebo ya muziki ya black market records ambayo inasimamia kazi zao za muziki.
 
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *