Entertainment

SAUTI SOL MBIONI KUJA NA ALBUM MPYA

SAUTI SOL MBIONI KUJA NA ALBUM MPYA

Kundi la muziki nchini sauti sol wametangaza mwezi ambao wataichia album yao ya sita tangu waanze safari yao ya muziki.

Kupitia barua ya wazi waliyoishare kwenye ukurasa wao wa instagram sauti sol wamesema album yao mpya itaingia sokoni mwezi mei mwaka wa 2022.

Wakali hao wa ngoma ya Suzzana wamesema kabla ya kuachia album yao mpya, wataachia singo yao mpya mwezi Disemba mwaka huu ambapo wamesema kwamba wataweka wazi tarehe ambayo wataachia project hiyo.

Sanjari na hilo wametusanua kwamba wanakuja na documentary yao iitwayo Alone Together ambayo itazungumzia changomoto ambazo wasanii wa kundi la sauti sol wamepitia tangu ujio wa janga la korona.

Kauli ya sauti sol inakuja mara baada ya kufanikisha tamasha lao la kimuziki liitwalo UK residency lilofanyika nchini uingereza mapema mwezi huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *