
Baby mama wa msanii Weasel, Sandra Teta amemtaka mke wa Jose Chameleone’, Daniella Atim akome kuingilia masuala ya mahusiano yake.
Daniella Atim amekuwa akiendesha kampeini ya kutaka haki itendeke kwa sandra teta ambaye aliripotiwa kushushiwa kipigo cha mbwa na mume wake Weasel manizo.
Lakini Sandra ameonekana kutopendezwa na kitendo cha Daniella kumtetea kwenye mitandao ya kijamii kwa kusema kwamba aache kufuatilia maisha yake ya ndoa na badala ashughulike na familia yake.
Hata hivyo Daniella Atim kupitia ukurasa wake wa Instagram amemjibu Sandra kwa kusema kwamba aache kujifanya ilhali anaumia moyoni kutokana na kichapo alichopewa na baby daddy wake Weasel Manizo.
Daniella ameenda mbali zaidi na kusema kwamba anaelewa sandra bado anapitia kipindi kigumu katika maisha yake, hivyo anapaswa kusaidiwa kimawazo ili arejee katika hali yake ya kawaida.