Others

SAVARA AMCHANA ERIC OMONDI, AMTAKA AACHE KUINGILIA WANAMUZIKI

SAVARA AMCHANA ERIC OMONDI, AMTAKA AACHE KUINGILIA WANAMUZIKI

Msaniii wa Sauti Sol, Savara Mudigi amepinga kauli ya mchekeshaji Eric Omondi kuwa wasanii wakenya hawana ubunifu wa kutengeneza matukio yatakayowafanya wazungumziwe kwenye tasnia ya muziki nchini.

Katika mahijiano yake hivi karibuni Savara amemtaka awache kujihusisha na masuala ya wanamuziki na badala yake awekeze muda wake kuboresha kazi yake ya ucheshi.

Sanjari na hilo Savara ameweka wazi matamanio yake ya kuingia kwenye siasa kwa kusema kuwa amekuwa akishinikizwa na watu wake wa karibu awanie wadhfa wa kisiasa lakini muda sahihi wa kufanya hivyo haujafika.

Utakumbuka Savara anafanya vizuri na album yake iitwayo Savage Level ambayo ina jumla ya nyimbo 14 ya moto

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *