
Prodyuza wa muziki Washington ameripotiwa kuvunjika vipande vipande kwa kuwa hana chochote zaidi ya hali mbaya ya kiuchumi.
Kupitia mitandao yake ya kijamii Washington ametoa ilani kwa wasanii wote aliofanya nao kazi kipindi cha nyuma kumlipa mirabaha ya kazi zake kutokana na kuyumba kiuchumi.
Hata hivyo mkali huyo kutoka Uganda ametoa makataa ya saa 24 kwa wasanii hao kumlipa haki yake la sivyo atafuta nyimbo zao kwenye majukwaa ya kuuza na kusikiliza muziki mtandaoni.
Kwa mujibu wa mitandao ya habari za burudani nchiniUganda, Washington anatajwa kuwa anapitia wakati mgumu kwa sasa kutokana na kutopata bookings kutoka kwa wasanii katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.