
Msanii Recho Ray amefunguka na kudai kwamba tasnia ya muziki nchini Uganda imesheheni ushirikina.
Katika mahojiano yake hivi karibuni Recho amesema nguvu za giza ndio chanzo ya baadhi ya wasanii wakongwe nchini humo kusalia kwenye muziki kwa muda mrefu.
Mrembo huyo amesema wasanii wengi wenye vipaji wamepotea kimuziki kutokana na baadhi ya wadau nchini Uganda kutumia hirisi kuua mafanikio yao.
Recho Ray ambaye ulimwengu wa muziki ulimfahamu mwaka 2018 kupitia wimbo wake uitwao “Who is Who” amekuwa akisuasua kwenye muziki wake bila kuachia hitsong yeyote.
Utakumbuka mrembo huyo sio msanii wa kwanza kudai kuwa kiwanda cha muziki nchini Uganda imetawala ushirikina, miezi kadhaa iliyopita msanii Nince Henry aliibuka na kuwatolea uvivu wasanii wote wanaoishi Makindye kwa tuhuma za kuwadhamini sana waganga wa kienyeji kwenye suala la kusafisha nyota yao ya muziki.