
Penzi la Harmonize na mchumba wake Kajala Masanja linazidi kushamiri kila kukicha na kuwafanya wenye makasiriko kusubiriwa wajinyonge.
Kupitia mfululizo wa Instastory zake, Harmonize amemwagia sifa kajala kwa kusema kuwa hakuna mwanamke mzuri kwa sasa anayemzidi mwanamama huyo.
Harmonize ambaye anafanya vizuri na ngoma zake mbili, “Nitaubeba” pamoja na “Amelowa” anasema kwamba penzi lao linazidi kuwa la moto kila siku na kama kuna mtu anatarajia litabuma basi avute kiti akae kwa sababu atasubiri sana.
Kauli ya Harmonize inakuja mara baada ya Kajala kuchora tattoo yake kwenye kidole cha pete; tattoo yenye herufi ya ‘R’ ikiwa ni herufi ya kwanza ya jina la Rajabu ambalo ndilo jina halisi la Harmonize.