
Rapa kutoka Marekani Coolio amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 59. Rafiki yake na meneja wa muda mrefu Jarez Posey ameithibitishia TMZ kwamba rapa huyo alifariki Jana Jumatano Jijini Los Angeles.
Kwa mujibu tovuti hiyo, Coolio alimtembelea rafiki yake na alipokwenda bafuni hakurudi tena. Rafiki yake baada ya kuona ukimya huo, alienda bafuni na kumkuta Coolio akiwa amelala sakafuni.
Rapa huyo ambaye jina lake halisi ni Artis Leon Ivey Jr inaripoti chanzo cha kifo chake ni Mshtuko wa Moyo lakini Polisi wamesema wanahunguza ziadi kuhusu tuko hilo.
Utakumbuka Coolio alipata umaarufu miaka ya 90 akiwa na nyimbo zake kama “Gangsta’s Paradise” na “Fantastic Voyage”