
Mwanakikundi wa Sauti Sol, Bien amekanusha madai yaliyoibuliwa na mchekeshaji Eric Omondi kuwa siri yake ya kuingia kwenye chati za Apple Music imetokana na kiki kwenye muziki wake.
Bien amesema hajawahi tengeneza matukio kwa ajili ya kutangaza muziki wake huku akisema mafanikio yake yamechangiwa na kujituma kwenye suala la kutoa muziki mzuri.
Msanii huyo ametoa changamoto kwa wasanii kuacha kutengeneza matukio yakuchafuana mtandaoni kwa lengo la kujitafuatia umaarufu na badala yake wawekeze muda wao kutoa muziki mzuri.
Bien ni msanii pekee kutoka Kenya aliyefanikiwa kuingiza nyimbo mbili kwenye chati za Apple Music Top 100. Nyimbo hizo ni pamoja na; Inauma ambayo ilikamata nafasi ya 40 huku “Dimension” aliyomshirikisha Fully Focus ikikamata nafasi ya 87.