
Video ya wimbo wa Willy Paul ‘Lalala ambao amemshirikisha Jovial imeondolewa kwenye mtandao wa YouTube kutokana na malalamiko ya hakimiliki.
Kwa sasa video hiyo ambayo ilikuwa na zaidi ya view laki 3 haipatikani kwenye mtandao huo kufuatia malalamiko ya hakimiliki kutoka kwa King Jones Official.
Hata hivyo Willy Paul hajatoa tamko lolote kuhusu kufutwa kwa video ya wimbo wa mambo yote youtube.
Ikumbukwe mtandao wa Youtube hauruhusu kutumia kazi au kionjo cha mtu mwengine bila makubaliano.