
Malikia wa mipasho Tanzania Khadija Kopa ambaye pia ni mama mzazi wa nyota wa muziki wa bongo fleva Zuchu, ameonesha kuchukizwa na ‘Komenti’ ya Romy Jons ambayo aliiandika kwenye ukurasa wa Instagram wa Zuchu. ‘Komenti’ hiyo iliandikwa baada ya Zuchu kuposti picha zake akita amevaa ‘Taiti fupi’, Romi aliandika, ‘’SHAPE NDIO HUNA MWAYA’.
Kupitia ‘komenti’ hiyo Khadija Kopa alishindwa kuvumilia na kuamua kutoa neno kumtaka Mwanae asiende Uturuki ambapo wengi huwa wanaenda kufanya upasuaji ili kuongeza umbo. Khadija aliandika, ‘’Wala usiende Uturuki mwanangu alonacho yeye huna na ulonacho wewe yeye hana huyo ndio Mungu @romyjons’’
Ikumbukwe kuwa Romy amekuwa mtu wa utani mwingi katika mitandao ya kijamii hasa katika komenti zake ambazo huwa anaandika kwa baadhi ya kurasa za watu mbalimbali.