
Mrembo King Alami amekiri kulitamani penzi la mpenzi wake wa zamani msanii Noti Flow ikiwa ni miezi kadhaa imepita tangu jini mkata kamba alipoingilia mahusiano yao na kuwatenganisha.
Kupitia video aliyochapisha kwenye ukarasa wake wa Instagram amesikika akijutia kuliacha penzi la Noti Flow kwa kusema kwamba tangu mahusiano yao yalipovunjika hajawahi pata furaha maishani kutokana na majuto ya vitendo vya usaliti alivyokuwa akishiriki kwa siri.
Hata hivyo amemuomba radhi Noti Flow pamoja na mashabiki zake kwa hatua ya kwenda kinyume na kiapo cha mahusiano yao huku akimsihi ampe nafasi nyingine ya kumpenda kwani hatokuja kumuacha asilani.
Utakumbuka King Alami na Noti Flow ambao wamekuwa gumzo nchini kwa kushiriki mapenzi ya jinsia moja, walikuwa kwenye mahusiano kwa muda wa miezi 6 kabla ya penzi lao kuingiwa na ukungu kwa madai ya usaliti.
Kipindi wawili hao wapo pamoja kama wapenzi walionyeshana upendo kiasi cha kila mmoja kuchora michoro ya tatoo kwenye miili yao lakini pia kuzawadiana vitu vya thamani ikiwemo gari kama njia ya kulifanya penzi lao libaki imara.