Entertainment

Nameless awajibu kisomo wanaomshinikiza kupata mtoto wa kiume

Nameless awajibu kisomo wanaomshinikiza kupata mtoto wa kiume

Msanii nyota nchini Nameless amewajibu walimwengu wanaomshinikiza kuzaa mtoto wa kiume kama njia ya kudhihirisha uanaume wake katika jamii.

Akimjibu shabiki mmoja aliyemtaka aweke mkakati wa kumpata mtoto wa kiume na mke wake Wahu kwenye mtandao wa Facebook, Nameless amesema anajivunia kuwa baba ya watoto wa kike na lengo lake kwa sasa ni kuwalea mabinti zake kwenye mazingira yatakayowapa fursa ya kuishi na watu vizuri.

Hitmaker huyo wa “Teamo” amewataka mashabiki kuacha kasumba ya kufuata mila zilizopitwa na wakati na badala yake wakumbatie utandawazi kama njia mojawapo ya kuendana na nyakati zilizopo. “Tafuta kijana boss…..Your legacy…..We Africans”, Shabiki aliandika kwenye mtandao wa Facebook ambapo Nameless alishuka kwenye uwanja wa comment na kuandika “”Saa zingine tunajiangusha na traditions that are outdated. Let’s evolve buana”

Ikumbukwe Nameless na Wahu ambao wamekuwa kwenye ndoa tangu mwaka 2005, kwa pamoja wamebarikiwa kuwapata mabinti watatu ambao ni Tumiso, Nyakio na Shiru ambaye alizaliwa juzi kati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *