Entertainment

WILLY PAUL: SIHITAJI SUPPORT YA WASANII WA KENYA KWENYE THE AFRICAN EXPERIENCE ALBUM

WILLY PAUL: SIHITAJI SUPPORT YA WASANII WA KENYA KWENYE THE AFRICAN EXPERIENCE ALBUM

Hitmaker wa Lenga msanii Willy paul ametoa ya moyoni baaada ya baadhi ya wasanii nchini kuzuzia kumpa support kwenye album yake ijayo  iitwayo The African Experience.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Willy Paul amewatolea uvivu wasanii ambao amewataja kama wanafiki kwa kusema kwamba ahitaji watu wa sampuli hiyo kumuunga mkono wakati huu anajianda kuiachia album yake mpya.

Bosi huyo wa Saldido ameenda mbali zaidi na kusema kwamba alizaliwa na atakufa pekee yake hivyo haitaji support ya mtu yeyote kwani Mungu yupo upande wake.

The Africa Experience album kutoka kwa mtu mzima Willy paul inatarajiwa kuingia sokoni rasmi Oktoba 24 mwaka ingawa hajatuambia  idadi ya nyimbo ambazo zitapstikana kwenye album hiyo.

Hii itakuwa ni Album yake ya pili, baada kuachia  album yake ya kwanza mwaka wa 2020 iitwayo songs of solomon ikiwa na jumla ya mikwaju kumi ya moto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *