
Mwanamitindo na aliyekuwa mke wa rapa Kanye West, Kim Kardashian ameonyesha kukasirishwa na kauli za aliyekuwa mume wake kuhusiana na tuhuma alizozitoa juu ya watu wenye asili ya kiyahudi.
Kupitia ukurasa wake wa twitter Kim Krdashian ameandika “Hotuba ya chuki siyo sawa au yenye udhuru, Nasimama pamoja na jamii ya watu wa kiyahudi na naomba kauli hizo za kigomvi na zenye chuki kuelekea kwa wayahudi zifikie mwisho haraka” – Kim Kardshian
Wiki iliyopita rapa Kanye West alitoa maneno ya chuki juu ya watu wenye asili ya kiyahudi huku akisema kuwa vyombo vya habari vya watu wa jamii ya kiyahudi vimekuwa vikitoa habari za kichonganishi zenye lengo la kuharibu jamii ya watu wa Marekani.
Watu wa jamii ya kiyahudi wamekasirishwa na kauli hizo za rapa huyo, huku wengi wakitishia kufungua kesi dhidi ya Kanye West