Entertainment

Ngoma ya Harmonize ‘Weed Language’ yarejeshwa Youtube

Ngoma ya  Harmonize ‘Weed Language’ yarejeshwa Youtube

Ngoma ya ‘Weed language’ ya staa wa muziki wa Bongo Fleva , Harmonize imerejeshwa tena katika mtandao wa Youtube wa msanii Konshens masaa kadhaa yaliyopita.

Harmonize jana kupitia ukurasa wake wa kijamii wa instagram aliahidi atauondoa wimbo huo kwenye mitandao yote ya kijamii baada ya kukiri kuwa maudhui ya wimbo huo yanakiuka maadili, mila na desturi pamoja na miongozo ya mamlaka za serikali nchini Tanzania.

Hata hivyo Harmonize alioundoa katika mtandao wake wa Youtube ila kwa sasa unapatikana katika chaneli ya Konshens aliyemshirikisha katika ngoma hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *