
Meneja wa wasanii nchini Uganda Abbey Musinguzi maarufu Abtex Promotions ametangaza kusitisha kufanya kazi na msanii Serena Bata.
Hii ni baada ya msanii huyo kuonekana akivuta sigara hadharani kitendo ambacho kilimkasirisha meneja wake huyo na kuchukua maamuzi magumu ya kutofanya naye kazi.
Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Abtex amesema licha ya kuvunja mkataba wake na Serena Bata, haitaathiri ratiba ya shows ambazo alikuwa amepangiwa na uongozi wake mwaka 2022.
Ikumbukwe Serena Bata amekuwa chini ya uongozi wa Abtex Promotions kwa kipindi cha miaka miwili.