Gossip

Akothee Achoshwa na Maswali ya Uhusiano Wake wa Nelly Oaks

Akothee Achoshwa na Maswali ya Uhusiano Wake wa Nelly Oaks

Msanii wa muziki kutoka Kenya, Akothee, ameonekana kukerwa na maswali ya mara kwa mara kutoka kwa baadhi ya mashabiki wake wanaoendelea kumuulizia aliyekuwa mpenzi wake, Nelly Oaks.

Kupitia kauli yake ya moja kwa moja, Akothee amewajibu mashabiki hao kwa ukali akisema, “Mumeskia ametangazwa amekufa?” kauli iliyoonyesha wazi kuchoshwa kwake na mada hiyo ambayo anaonekana hataki kuirudia tena.

Akothee ameonekana kusisitiza kuwa kila mtu ana maisha yake na kwamba uhusiano wake wa zamani haupaswi kuendelea kuwa mjadala wa kila siku mitandaoni.

Mwanamama huyo, ameeleza kuwa mashabiki wanapaswa kuzingatia mambo ya maana zaidi badala ya kuendelea kuchimba masuala aliyoyaacha nyuma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *