Mtangazaji na mdau wa burudani, Mwijaku, amezua gumzo mitandaoni baada ya kumtolea uvivu Chief Godlove, akigusia suala la umiliki wa magari ya kifahari bila kuwa na maegesho binafsi.
Kupitia clip aliyoposti akiwa nyumbani kwake, Mwijaku ameonyesha magari yake yakiwa yameegeshwa kwenye parking ya nyumba yake, akisema haiwezekani mtu kudai kumiliki magari ya kifahari ilhali hana parking yake mwenyewe kwa sababu anaishi nyumba za kupanga.
Kwa mujibu wa Mwijaku, umiliki wa magari ya thamani kubwa unapaswa kwenda sambamba na makazi yenye maegesho salama, akisisitiza kuwa hilo ni suala la mipango ya maisha na si kujionyesha tu.
Kauli hiyo imekuja baada ya Chief Godlove juzi kati kuonekana kwenye clip nyingine akionesha mashabiki wake gari lake lililovunjwa kioo. Katika clip hiyo, Godlove alionekana ameegesha gari lake kwenye parking iliyojaa magari mengi, hali iliyozua maswali na mjadala mkubwa mitandaoni.