LifeStyle

Akothee Ataka Jamii Iache Kuingilia na Kukosoa Mtindo Wake wa Mavazi

Akothee Ataka Jamii Iache Kuingilia na Kukosoa Mtindo Wake wa Mavazi

Msanii wa muziki kutoka Kenya, Akothee, amewataka wakosoaji wake kuacha kuingilia mtindo wake wa mavazi na maisha binafsi, akisema lawama nyingi zinazomkabili zinatoka kwa watu wasioishi kulingana na maadili wanayoyahubiri mitandaoni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Akothee ameweka wazi kuwa hataki kuelekezwa jinsi ya kuvaa na watu anaodai wanaficha maovu yao binafsi nyuma ya pazia la maadili ya kijamii. Ameeleza kuwa kuna watu wanaojifanya walinzi wa maadili ilhali familia zao zinakumbwa na matatizo makubwa kama ulevi, usaliti katika ndoa na kuvunjika kwa familia.

Msanii huyo amesisitiza kuwa sanaa ni njia ya kujieleza na kwamba jamii inapaswa kujifunza kuheshimu uhuru wa wasanii badala ya kuwahukumu kwa misingi ya mitazamo binafsi. Aidha, amewataka wanaomkosoa waangalie kwanza mienendo yao kabla ya kumshambulia hadharani.

Kauli hiyo ya Akothee imekuja baada ya kukosolewa vikali na baadhi ya wanajamii kufuatia kusambaa kwa vipande vya video ya wimbo wake mpya uitwao Society. Video hiyo inaonyesha mavazi yanayobana na kufichua sehemu nyeti za mwili wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *