Msanii asiyeishiwa na matukio kila leo, Akothee, ameibuka na taarifa njema kwa mashabiki wake baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini kufuatia kulazwa kwa muda kutokana na matatizo ya tumbo.
Akizungumza mara baada ya kutoka hospitalini, Akothee ametoa shukrani za dhati kwa wote waliomuombea apone haraka na waliomtumia salamu za faraja wakati wa kipindi hicho kigumu. Ameeleza kuwa maombi na upendo wa mashabiki wake yamempa nguvu na matumaini makubwa ya kupona.
Hata hivyo, amewashangaza wengi baada ya kufichua kuwa kulikuwa na baadhi ya watu waliotumia mitandao ya kijamii kumtakia mabaya, akiwemo wanaodaiwa kumtakia kifo. Amesema tukio hilo halikumvunja moyo, bali limempa sababu zaidi ya kuthamini wale wanaomuunga mkono kwa dhati.
Akothee alikuwa amelazwa hospitalini baada ya kukumbwa na matatizo ya tumbo yaliyomfanya kupata maumivu makali. Kwa sasa, anasema afya yake imeimarika na ameanza kuendelea vyema chini ya uangalizi wa madaktari.