Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, BillNass, ameibuka tena kwenye mitandao ya kijamii baada ya ukimya wa muda kufuatia tukio la ghasia za Uchaguzi Mkuu lililosababisha duka lake la Nenga Tronix kuchomwa moto.
Kupitia WhatsApp Status, BillNass alichapisha video fupi inayoonyesha baadhi ya mali zilizookolewa, ikiwemo simu, laptop, na pesa taslimu zilizobaki salama licha ya duka kuteketea.
Katika video hiyo, msanii huyo aliambatanisha emoji za mikono ya maombi 🙏🏾🙏🏾 kama ishara ya kumshukuru Mungu kwa kunusuru kilichoweza kuokolewa.
BillNass amekuwa kimya kwenye mitandao mengine, ikiwa ni pamoja na kuufunga ukurasa wake wa Instagram, hatua aliyochukua mara tu baada ya tukio hilo la kusikitisha.