
Mwanamuziki wa nyimbo za injili nchini Guardian Angel anazidi kufanya vizuri kupitia mauzo ya mtandaoni na Album yake ” Victory ” ambayo tayari ina takriban miezi miwili tangu itoke rasmi.
Goods ni kwamba Album ya “Victory” imefanikiwa kufikisha jumla ya Streams millioni moja kwenye mtandao wa kusikiliza na kupakua muziki wa Boomplay Kenya.
Album ya “Victory” iliachiwa rasmi Novemba 11 mwaka 2021 ikiwa na jumla ya ngoma 10 ya moto na ni album ya pili kwa mtu mzima guardian angel tangu aanze safari yake ya muziki baada ya Thanks for Coming iliyotoka mwezi mei mwaka 2021