
Bado sakata la mwanamuziki Marioo kudaiwa kumuomba Diamond Platnumz amsaini katika record label ya WCB Wasafi linazidi kuibua mapya mengine, baada ya aliyekuwa shemeji wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Msizwa kufichua kuwa jambo hilo limegeuzwa na kwamba Diamond Platnumz ndiye aliyekuwa akitaka kumsani Marioo na sio Marioo kutaka kusainiwa na Diamond.
Msizwa ambayee kupitia ukurasa wake wa Instagram ameeleza kuujua ukweli, amedai kwamba alikuwa sehemu ya shuhuda wakati wa mazungumzo ya Diamond Platnumz kutaka kumsaini Marioo kipindi wapo wasafi village, ambapo Marioo alionesha kutoafiki jambo hilo kwa wakati huo kiasi cha kuomba ushauri kutoka kwake.
Hata hivyo Msizwa ameeleza kuwa kama kuna siku nyingine wawili hao waliongea kuhusu hilo jambo na yeye hakuwepo ni sawa ,lakini kama ni kipindi hicho alicho sema Baba Levo basi yeye alikuwepo kama shuhuda pamoja na Baba Levo pia.