
Timu ya Taifa ya Argentina imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Dunia baada ya kuitandika Australia 2-1 katika mchezo uliokuwa wa kusisimua
Nahodha Lionel Messi akiwa kwenye kiwango bora zaidi alipachika bao moja kabla ya Alvarez kutumia vyema makosa ya mlinda lango wa Australia kupachika bao la pili kwa Argentina
Sasa Argentina watakutana na Uholanzi katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo na kurudisha kumbukumbu ya mwaka 1998 timu hizo zilipokutana kwenye hatua kama hiyo na Uholanzi kushinda 1-0.
Ikumbukwe timu ya Taifa ya Uholanzi iliilaza Marekani 3-1 katika mchezo wa hatua ya 16 bora.