
Msanii nyota nchini Arrow Boy ameshindwa kuvumilia watu wanaomkosoa baby mama wake Nadia Mukami kutokana na mavazi aliyovalia juzi kati kwenye onesho lake huko Meru.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Arrow Boy ameshangazwa namna watu wanavyomshambulia Nadia Mukami kwenye mitandao ya kijamii kwa mambo yasiokuwa na msingi huku akisema kuwa huenda ni mafanikio ya msanii huyo ndio imepelekea baadhi ya watu kuanza kumchukia.
“Watu huku nje roho zao zimejaa machungu just ready to explode like a time bomb….Why too much hate?” Ameandika Instagram.
Hitmaker huyo wa Enjoy amesema watu waache kumuonea Nadia Mukami wivu kwenye muziki wake kwa kuwa anazidi kuandika historia ya kipekee ambayo hajawahi fikiwa na msanii yeyote wa kike nchini.
“As you keep hating, others are making history….Tuseme tu ukweli which female artist in Kenya has pulled a move @NadiaMukami pulled over the weekend in Meru since Kenya izaliwe? Hakuna…” Ameongeza Arrow Boy