
Klabu ya Arsenal iliibamiza Manchester city kipigo cha magoli matano kwa moja kwenye mechi ya ligi nchini England iliyochezwa leo ugani Emirates.
Magoli ya Arsenal yalifungwa na Martin Odergard, Thomas Partey, Myles Lewis Skelly, Kai Havertz na Ethan Nwaneri dakika ya 2, 56, 62, 76 na 90+3 huku Earling Haaland akifungia Manchester city bao pekee la kufutia machozi dakika ya 55.
Kwa matokeo hayo Arsenal anashikilia nafasi ya pili kwa pointi 50 nyuma ya vinara Liverpool ambao wana pointi 56 kwenye msimamo wa ligi kuu England. Manchester city iko katika nafasi ya nne na pointi ya 41.
Kwengineko Manchester United imekubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Crystal Palace katika dimbani la Old Trafford. Mabao ya mawili ya Jean Mateta dakika ya 64 na 89 yalitosha kabisa kuharibu wikiendi ya vijana wa Ruben Amorin, Manchester United iko nafasi ya 13 ikiwa na alama 29 baada ya michezo 24 kwenye Ligi Kuu ya Uingereza EPL
Kwenye matokeo mengine iliyochezwa hii leo, Totenham Hotspurs akiwa ugenini dhidi ya Brentford alipata ushindi wa magoli mawili bila jibu. Magoli ya Spurs yalifungwa na Vitaly Janelt ambaye alijifunga dakika ya 29 na PaperΒ Matar Sarr dakika ya 87. Kwa matokeo hayo, Spurs anashikilia nafasi 14 ya na pointi 27 nyuma ya Brentford ambao wanashikilia nafasi 11 ya na pointi 31 kwenye msimamo wa ligi kuu nchini England.