Muonekano Mpya wa Upara wa Harmonize Wazua Mjadala

Muonekano Mpya wa Upara wa Harmonize Wazua Mjadala

Staa wa muziki kutoka Tanzania, Harmonize, ameibua gumzo mitandaoni baada ya kufichua muonekano wake mpya wa upara muda mfupi tu baada ya kuwasili nchini Kenya kwa shughuli zake za kimuziki. Picha zake zikimuonyesha akiwa na mtindo huo mpya zilisambaa kwa kasi, na mashabiki wengi wameanza kutoa maoni mseto kuhusu hatua hiyo ya ghafla. Baadhi ya […]

Read More
 Burna Boy: “Sikulazimisha Mtu Kunipenda, Nataka Mashabiki Wenye Pesa”

Burna Boy: “Sikulazimisha Mtu Kunipenda, Nataka Mashabiki Wenye Pesa”

Mwanamuziki nyota wa Nigeria, Burna Boy, ameibua gumzo mitandaoni baada ya kutoa kauli tata akisema kwamba hakumlazimisha mtu yeyote kuwa shabiki wake na kwamba anawapendelea zaidi mashabiki wenye pesa. Kupitia Instagram Live, Burna Boy, amesisitiza kuwa hakuna mtu anayelazimishwa kufuatilia muziki wake, huku akiongeza kuwa anathamini mashabiki wanaoonyesha uaminifu kwa kazi yake na wanaoweza kumudu […]

Read More
 Wakenya Watishia Kususia Shoo za Harmonize

Wakenya Watishia Kususia Shoo za Harmonize

Baadhi ya Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wameonyesha wazi kutoridhishwa na msanii wa Bongo Fleva, Harmonize, wakitishia kususia shoo zake zote zitakazofanyika nchini Kenya baada ya msanii huyo kuwasili nchini humo kwa ziara ya kikazi. Wengi wao mtandaoni wamesema hawatohudhuria shoo zake, wakimtuhumu kwa kukaa kimya wakati Watanzania walikumbwa na madhila ya kisiasa. Baadhi wamesisitiza […]

Read More
 Harambee Stars Yacharazwa 8–0 na Senegal Uturuki

Harambee Stars Yacharazwa 8–0 na Senegal Uturuki

Timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, imepata matokeo mabaya zaidi katika historia ya mechi zake za kirafiki baada ya kulala 8–0 dhidi ya miamba wa Afrika Senegal, kwenye mchezo uliopigwa jana usiku nchini Uturuki. Mchezaji nyota wa Al-Nassr na zamani wa Liverpool, Sadio Mane, aling’ara kwa kufunga hat-trick, huku mshambulizi wa Bayern Munich Nicolas […]

Read More
 Jeshi la Polisi Thibitisha Kifo cha Mchekeshaji Maarufu MC Pilpili

Jeshi la Polisi Thibitisha Kifo cha Mchekeshaji Maarufu MC Pilpili

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limethibitisha kifo cha mchekeshaji maarufu wa Tanzania MC Pilpili anayefahamika kama Emmanuel Mathias Matebe, kilichotokea Novemba 16, 2025 katika Kituo cha Afya Ilazo jijini Dodoma. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, ACP William Mwanafupa, amesema marehemu alifikishwa kituoni hapo majira ya mchana akiwa katika hali mbaya na alifariki […]

Read More
 Mke wa Guardian Angel Afunguka Kuhusu Matusi Mtandaoni

Mke wa Guardian Angel Afunguka Kuhusu Matusi Mtandaoni

Mke wa mwimbaji wa Injili Guardian Angel, anayefahamika kama Esther Musila, ameapa kupambana vikali na wakosoaji wake mtandaoni hadi mwisho wa dunia. Kupitia ukurasa wake wa TikTok, Musila amesisitiza kuwa hatakubali kunyamaza huku akivunjiwa heshima mtandaoni bila kujibu. Mwanamama huyo ameonyesha hasira yake kwa watu wanaojiona wana uwezo wa kudhibiti maisha ya watu wengine, akisema […]

Read More
 Eddy Kenzo Afunguka Sababu ya Kukataa Mikataba Kubwa ya Muziki

Eddy Kenzo Afunguka Sababu ya Kukataa Mikataba Kubwa ya Muziki

Mwanamuziki nyota kutoka Uganda, Eddy Kenzo, amefunguka kuhusu sababu za kukataa kusaini mikataba na kampuni kubwa za muziki duniani, zikiwemo Sony Music na Universal Music Group. Kenzo, ambaye ni miongoni mwa wasanii waliotukuka zaidi nchini Uganda na mwenye tuzo kama BET Award pamoja na uteuzi kadhaa wa Grammy, amesema amepewa ofa nyingi lakini amezikataa kwa […]

Read More
 Rapa Toxic Lyrikali Adharau Diss Track ya Wakuu Music

Rapa Toxic Lyrikali Adharau Diss Track ya Wakuu Music

Rapa anayeongoza katika chati za muziki nchini Kenya, Toxic Lyrikali, amepuuza kwa dharau ‘diss track’ iliyomlenga iliyotolewa na kundi la Wakuu Music, akieleza kuwa hana muda wa kujibu migogoro inayoendeshwa na wivu na chuki kutokana na mafanikio yake. Kupitia Instagram Live, Toxic Lyrikali amesema wazi kuwa hawezi kamwe kujibu diss track kutoka kwa wasanii ambao […]

Read More
 Akothee Amkingia Kifua Winnie Odinga Dhidi ya Ubaguzi wa Kisiasa

Akothee Amkingia Kifua Winnie Odinga Dhidi ya Ubaguzi wa Kisiasa

Mwanamuziki na mfanyabiashara maarufu nchini Kenya, Akothee, amejitokeza kutoa msimamo mkali, akimkinga kifua Mbunge wa EALA, Winnie Odinga dhidi ya kile anachokiita ubaguzi wa kisiasa. Akothee amekemea vikali wale wanaomdhalilisha Winnie Odinga, binti ya hayati Raila Odinga, kwa kigezo cha kuwa hajaingia kwenye ndoa. Kupitia ujumbe wake kwenye mitandao ya kijamii, Akothee, amesisitiza kuwa sifa […]

Read More
 Alien Skin Awashutumu Wasanii Wanaoshiriki Kampeni za Museveni

Alien Skin Awashutumu Wasanii Wanaoshiriki Kampeni za Museveni

Msanii mwenye utata mkubwa nchini Uganda, Alien Skin, ametoa matamshi makali dhidi ya wasanii wanaoendelea kutumbuiza kwenye kampeni za Rais Yoweri Museveni baada ya kujiondoa kwenye misafara ya kampeni kutokana na malipo duni. Akiwa jijini Kampala, Alien Skin amewakashifu wasanii hao, akisema juhudi zao hazina nguvu kwa sababu muziki wake ndio unaoamsha umati na kuongeza […]

Read More
 Thee Pluto Alalamikia Kunyimwa Kumwona Binti Yake Zoey

Thee Pluto Alalamikia Kunyimwa Kumwona Binti Yake Zoey

Mwanamitandao maarufu nchini Kenya, Thee Pluto, ameshindwa kujizuia na kuibua hisia kali mitandaoni baada ya kudai kwamba amekuwa akinyimwa fursa ya kumwona binti yake, Zoey. Kwenye mahojiano na Obinna TV, Pluto amesema hali hiyo imekuwa ikimuumiza kwa muda mrefu huku akimtaja mama mzazi wa Felicity, ambaye ni mama mkwe wake, kama chanzo kikuu cha mgogoro […]

Read More