Ali Kiba Aomba Msamaha Watanzania kwa Kujihusisha na Siasa

Ali Kiba Aomba Msamaha Watanzania kwa Kujihusisha na Siasa

Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva Alikiba ameomba radhi kwa Watanzania kufuatia hasira zilizozuka baada ya yeye kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa kampeni za uchaguzi wa hivi karibuni. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Alikiba amewaomba radhi Watanzania kwa kuwaumiza kupitia msimamo wake wa kisiasa na kuwapa pole wale wote waliopoteza maisha au kujeruhiwa […]

Read More
 Gloria Ntazola Afichua Ameamua Kujitenga na Familia Yake kwa Sababu za Kihisia

Gloria Ntazola Afichua Ameamua Kujitenga na Familia Yake kwa Sababu za Kihisia

Mrembo na mtayarishaji wa maudhui Gloria Ntazola amefichua kuwa ameamua kujitenga na familia yake, akisema amechoshwa kihisia kutokana na kutothaminiwa na kukosa sapoti ya kihisia kutoka kwao. Kupitia ujumbe aliouchapisha mtandaoni, Gloria alisema kuwa wengi wa ndugu zake humtafuta tu wanapohitaji pesa, lakini hawajali kuhusu hali yake au ustawi wake binafsi. Ameeleza kuwa hali hiyo […]

Read More
 Watanzania Waanza Ku-unfollow Wasanii Waliomuunga Mkono Rais Samia Suluhu

Watanzania Waanza Ku-unfollow Wasanii Waliomuunga Mkono Rais Samia Suluhu

Baadhi ya Watanzania wameanzisha kampeni kubwa ya mitandaoni ya kuwa-unfollow wasanii maarufu waliomuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika harakati zake za kurejea madarakani. Miongoni mwa waliokumbwa na wimbi hilo ni staa wa Bongo Fleva Diamond Platnumz, ambaye inaripotiwa amepoteza zaidi ya wafuasi 100,000 ndani ya saa 12 pekee. Msanii mwingine anayelengwa ni Harmonize, ambaye […]

Read More
 Msanii Shilole Asamehe Walioharibu Biashara yake, Asema Hatarudi Nyuma Kisiasa

Msanii Shilole Asamehe Walioharibu Biashara yake, Asema Hatarudi Nyuma Kisiasa

Msanii na mfanyabiashara wa Tanzania, Shilole, amezungumza kwa mara ya kwanza baada ya mgahawa wake maarufu Shishi Food kuchomwa moto na waandamanaji wakati wa vurugu zilizoshuhudiwa nchini hivi karibuni. Kupitia ujumbe Instagram, Shilole amewatakia pole wote waliofikwa na misiba, majeraha, au hasara kutokana na machafuko hayo, akisisitiza kuwa kurudishiana maumivu si utu na kwamba tofauti […]

Read More
 Chameleone Akanusha Kulipwa na Rais Museveni Kufamnyia Kampeini

Chameleone Akanusha Kulipwa na Rais Museveni Kufamnyia Kampeini

Msanii mkongwe kutoka nchini Uganda, Jose Chameleone, amekanusha madai kwamba wasanii wanaomuunga mkono Rais Yoweri Kaguta Museveni wanalipwa fedha nyingi. Akizungumza na kituo cha televisheni nchini humo, Chameleone ambaye yuko kwenye kampeni ya kumpigia upatu Museveni pamoja na wasanii wenzake Bebe Cool na Eddy Kenzo, amesema kuwa anafanya hivyo kwa hiari yake kama ishara ya […]

Read More
 Mwijaku Awataka Watanzania Kudumisha Amani Badala ya Kulaumiana

Mwijaku Awataka Watanzania Kudumisha Amani Badala ya Kulaumiana

Mtangazaji maarufu wa Tanzania Mwijaku ameomba radhi kwa Watanzania kwa kusimama na kuunga mkono serikali wakati wa kampeni za uchaguzi wa Oktoba 29. Kupitia sauti iliyosambaa mitandaoni, Mwijaku amesema anatambua kuwa baadhi ya kauli zake wakati wa kampeni ziliwaumiza wananchi, hasa ikizingatiwa machafuko yaliyofuata baada ya uchaguzi huo. Amesema lengo lake halikuwa kuwagawanya Watanzania bali […]

Read More
 Mangi Kimambi Ataka Watanzania Kususia Shows za Wasanii Waliounga Mkono Rais Samia Hassan

Mangi Kimambi Ataka Watanzania Kususia Shows za Wasanii Waliounga Mkono Rais Samia Hassan

Mwanaharakati maarufu wa Tanzania Mangi Kimambi ametoa wito kwa Watanzania kususia maonyesho na matamasha ya wasanii wanaoonekana kuunga mkono serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan. Kupitia mitandao ya kijamii, Mangi amesema wasanii hao wamekuwa wakikaa kimya au hata kuwatetea viongozi licha ya wananchi kukabiliana na changamoto nyingi ikiwemo ukandamizaji wa haki za kiraia na vurugu […]

Read More
 Mchekeshaji Nasra Yusuf Apigwa Block na Zuchu Instagram Kisa Maandamano Tanzania

Mchekeshaji Nasra Yusuf Apigwa Block na Zuchu Instagram Kisa Maandamano Tanzania

Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Nasra Yusuf, amedai kwamba msanii wa Bongo Fleva Zuchu amempiga block kwenye mtandao wa Instagram. Nasra amesema hatua hiyo imekuja baada ya yeye kushinikiza wasanii wa Tanzania kuzungumza wazi kuhusu hali ya maandamano na ukatili unaoripotiwa nchini humo. Kwa mujibu wa Nasra, lengo lake lilikuwa kuwataka mastaa kutumia ushawishi wao kukemea […]

Read More