Binti Aliyemlilia Oga Obinna Mtandaoni Apata Mwaaliko wa Chakula

Binti Aliyemlilia Oga Obinna Mtandaoni Apata Mwaaliko wa Chakula

Mtangazaji na mchekeshaji maarufu Oga Obinna ameahidi kumpeleka lunch date binti aliyesambaa mitandaoni baada ya kuonekana akimwaga machozi akieleza wazi mapenzi yake kwake kupitia video iliyosambazwa mitandaoni. Binti huyo alionekana akieleza jinsi anavyompenda Obinna kwa moyo wake wote na kumwomba ampe nafasi ya kuwa naye, jambo lililozua maoni mseto mitandaoni. Obinna kupitia ukurasa wake wa […]

Read More
 Diamond Platnumz Avunja Ukimya Kufuatia Tetesi za Kukimbilia Dubai

Diamond Platnumz Avunja Ukimya Kufuatia Tetesi za Kukimbilia Dubai

Msanii nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, amejitokeza kukanusha madai yaliyosambaa mtandaoni kwamba amekimbilia Dubai kufuatia machafuko yaliyoshuhudiwa nchini Tanzania baada ya uchaguzi wa Oktoba 29. Tetesi hizo zilidai kuwa Diamond na familia yake waliondoka nchini Tanzania kwa hofu ya kushambuliwa, baada ya baadhi ya biashara za wasanii waliomuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kuripotiwa […]

Read More
 Rayvanny Atoa Onyo Kali Kwa Anaendesha Akaunti Feki Facebook kwa Jina Lake

Rayvanny Atoa Onyo Kali Kwa Anaendesha Akaunti Feki Facebook kwa Jina Lake

Msanii wa Bongo Fleva, Rayvanny, ametoa onyo kali kwa mtu anayejifanya yeye kwenye ukurasa wa Facebook ulioidhinishwa (verified), wenye wafuasi zaidi ya milioni 3.4, baada ya akaunti hiyo feki kutumia jina lake kuposti picha na video za matukio ya kusikitisha yanayoendelea nchini Tanzania. Kupitia instastory zake, Rayvanny alionekana mwenye hasira akimtahadharisha mtu huyo kuacha mara […]

Read More
 Khalif Kairo na Phoina Wanaswa Wakipigana Mabusu Hadharani

Khalif Kairo na Phoina Wanaswa Wakipigana Mabusu Hadharani

Mfanyabiashara mwenye utata Khalif Kairo na mrembo maarufu wa mitandao ya kijamii Phoina wamezua gumzo mitandaoni baada ya kunaswa kwenye video wakionyeshana mapenzi hadharani. Katika video hiyo, ambayo imesambaa kwa kasi mitandaoni, wawili hao walionekana wakiwa kwenye moja ya kumbi za burudani jijini Nairobi, wakishindwa kujizuia na kuanza kupigana mabusu mbele ya umati wa watu. […]

Read More
 Barak Jacuzzi Amshinda Actually Lumu katika Pambano la Celebrity Fight Night

Barak Jacuzzi Amshinda Actually Lumu katika Pambano la Celebrity Fight Night

Msanii wa muziki wa hip-hop nchini Kenya Barak Jacuzzi ameibuka mshindi dhidi ya Youtuber Actually Lumu katika pambano lililosubiriwa kwa hamu la Celebrity Fight Night Showdown lililofanyika wikiendi hii iliyomalizika jijini Nairobi. Mashabiki walijitokeza kwa wingi kushuhudia pambano hilo lililokuwa na msisimko mkubwa, ambapo Barak Jacuzzi alionyesha umahiri na nguvu za kipekee ulingoni, akimdhibiti mpinzani […]

Read More
  Msanii Stevo Simple Boy Abarikiwa Mtoto wa Kiume na Mpenzi Wake Brenda

 Msanii Stevo Simple Boy Abarikiwa Mtoto wa Kiume na Mpenzi Wake Brenda

Msanii wa muziki kutoka nchini Kenya, Stevo Simple Boy na mpenzi wake Brenda, wamekaribisha mtoto wao wa kwanza, mvulana waliompa jina Dragon Junior. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Stevo ameshiriki picha akiwa pamoja na Brenda wakimkumbatia mtoto wao mchanga na kufahamisha mashabiki kuwa Dragon Junior amezaliwa salama. Pia ametoa shukrani kwa wafuasi wake kwa sapoti […]

Read More
 Karole Kasita Asema Hana Mpango wa Kuolewa

Karole Kasita Asema Hana Mpango wa Kuolewa

Mwanamuziki wa Dancehall kutoka nchini Uganda, Karole Kasita, amefunguka kuwa hana mpango wa kuingia kwenye ndoa kwa sasa, akisisitiza kuwa nguvu zake zote kwa sasa amezielekeza kwa mtoto wake na kazi ya muziki. Karole, ambaye alijifungua mtoto wake wa kwanza takribani miaka mitatu iliyopita, amefafanua kuwa ingawa hajaolewa na baba wa mtoto wake, lakini amemshukuru […]

Read More
 Rapa Rose Ree Atoa Wito wa Amani Kufuatia Machafuko ya Uchaguzi Nchini Tanzania

Rapa Rose Ree Atoa Wito wa Amani Kufuatia Machafuko ya Uchaguzi Nchini Tanzania

Rapa kutoka nchini Tanzania, Rose Ree, ameelezea huzuni yake kufuatia machafuko yanayoripotiwa kutokea nchini humo baada ya uchaguzi mkuu uliokumbwa na utata mkubwa. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, msanii huyo ameandika ujumbe mzito akionesha masikitiko yake kwa hali ilivyo nchini Tanzania, akisema kwamba moyo wake unaumia kutokana na machafuko hayo na kwamba bado analipenda taifa […]

Read More
 VJ Patelo Amshambulia Toxic Lyrikali kwa Kuishi Maisha ya Feki

VJ Patelo Amshambulia Toxic Lyrikali kwa Kuishi Maisha ya Feki

Msanii wa Arbantone VJ Patelo ameibua upya mzozo na msanii wa hip-hop Toxic Lyrikali, akimtuhumu kuishi maisha bandia na kukosa ubunifu katika muziki wake. Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii, Patelo amedai kuwa Lyrikali hudanganya katika mashairi ya muziki kuhusu utajiri na mali anazomiliki, ikiwemo madai ya kuwa na gari la kifahari aina ya […]

Read More