
Wasanii Avril na Tanasha Donna wameonesha ghadhabu zao kwa kampuni ya Zuku kutokana na huduma duni ya mtandao.
Kupitia mitandao yao ya kijamii wasanii hao wawili wametoa malalamiko yao kwa kampuni hiyo kufuatia kukosa huduma ya mtandao kwa kipindi cha siku tatu mfululizo.
Hata hivyo wameichana kampuni ya Zuku kwa hatua ya kuwa na wahudumu wasiowajibikia majukumu ya kujibu simu za wateja wao wakati wa dharura huku wakitshia kuhamia makampuni mengine ambayo yanatoa huduma ya mtandao.