Entertainment

Baba Levo ahaidi kumsaidia Anjella baada ya Harmonize kumkimbia

Baba Levo ahaidi kumsaidia Anjella baada ya Harmonize kumkimbia

Sakata la Harmonize na msanii wake Anjella limemgusa mwanamuziki wa Bongofleva Baba Levo ambaye ameweka wazi atamsaidia msanii huyo matibabu ya mguu wake kwa kumpeleka India na Qatar.

Kupitia ukurasa wake instagram Baba Levo amesema “Dada Anjella Naitwa Baba Levo NAKUHAKIKISHIA UTAENDA QATAR NA UTAENDA INDIA PIA KWA AJILI YA MATIBABU …!! KIRANDAGE PAMOJA NA BANGE ZAKE ILA AMEKUTOA MBALI SEMA TU AMEISHIWA HELA KWA SASA

NA HII NI KWASABABU YA KUTAKA KUSHINDANA NA DIAMOND PLATINUMZ AMEJIKUTA AMEFILISIKA KABISA…!”

Ikumbukwe, jana Harmonize kupitia insta story yake aliweka ujumbe akitaka mtu yeyote anaeweza kuendeleza kipaji cha Anjella asisite kujitokeza kwa ajili ya kumsaidia msanii huyo.

Hata hivyo, kwenye ujumbe huo boss huyo wa Konde Gang hakuweka wazi kama lebo yake ndio imeachana rasmi na Anjella.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *