LifeStyle

Baba Levo Amzawadia Mke Wake Range Rover

Baba Levo Amzawadia Mke Wake Range Rover

Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini ambaye pia ni msanii wa muziki, Baba Levo, amegusa hisia za wengi baada ya kumzawadia mke wake gari jipya aina ya Range Rover kama ishara ya shukrani kwa mchango wake mkubwa katika safari yake ya kisiasa.

Akizungumza kuhusu zawadi hiyo, Baba Levo amesema mke wake alikuwa nguzo muhimu wakati wa kampeni zake za kuwania ubunge wa Kigoma Mjini, akimhudumia, kumpa moyo na kusimama naye bega kwa bega katika kipindi kigumu cha kampeni.

Mkali huyo wa Shusha, amesema zawadi hiyo siyo tu gari, bali ni ishara ya kuthamini juhudi, uvumilivu na msaada wa dhati alioupata kutoka kwa mke wake tangu mwanzo wa harakati zake za kisiasa hadi kufanikisha ushindi.

Instagram/Baba Levo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *