Staa wa muziki Bahati na mkewe Diana Marua wamezua gumzo mitandaoni baada ya kubainika kuwa wameacha kufuatana (unfollow) kwenye mtandao wa Instagram.
Hatua hiyo imewashangaza mashabiki wao wengi, hasa ikizingatiwa kuwa wawili hao wamekuwa wakionekana kama wanandoa wanaoheshimika zaidi kupitia mitandao ya kijamii.
Kinachozidi kuzua maswali ni kwamba kila mmoja wao amefuta picha zote zilizokuwa kwenye kurasa zao za Instagram, huku ukurasa wa Diana Marua ukionekana kuwa mtupu kabisa bila hata picha moja.
Hatua hii imewafanya mashabiki na wadau wa burudani kuanza kubashiri huenda kuna jambo zito linaendelea ndani ya ndoa yao. Kwa sasa, macho na masikio ya mashabiki yako kwa wawili hao wakisubiri kauli rasmi itakayoweka wazi ukweli wa kile kinachoendelea.