
Baba mzazi wa Rapa Tory Lanez ameonekana kutoridhishwa na maamuzi ya mahakama kumkuta na hatia mwanaye kwenye shtaka la kumpiga risasi Megan Thee Stallion ambapo huenda akahukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka 20 gerezani.
Akiwa nje ya Mahakama, mzee huyo Sonstar Peterson, amemshtumu rapa Jay-Z pamoja Roc Nation kuwa wamehusika nyuma ya pazia kwenye maamuzi hayo.
Familia nzima ya Tory Lanez imeonesha kuwa na hasira na Jay-Z pamoja na Beyonce wakidai kufanyiwa mchezo mchafu na familia hiyo. Jay-Z anatajwa kuhusika hadi kwenye kulipa gharama za kuendesha kesi hiyo.
Ikumbukwe mwezi Juni mwaka 2022, Jay-Z alitangaza kumsaini Megan Thee Stallion ndani ya Roc Nation.