
Baby mama wa mchekeshaji Mulamwah, Carol Sonnie amesikitisha na namna baadhi ya watu ambao wameanza kufanya mzaha na ishu ya kuachana na mchekeshaji huyo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Carol Sonnie ameandika waraka mrefu akiwataka wanaotumia picha yake wakidai kwamba wanachumbia kushusha picha hizo ujumbe ambao umetafsiriwa unamlenga mchekeshaji Propesa ambaye juzi kati alipost picha ya mrembo huyo akidaiwa kuwa ni wapenzi.
Mrembo huyo ambaye ni mtoto wa mmoja amesema kitendo hicho sio cha kingwana ikizingatiwa kuwa inamharibia sifa mbele ya umma pamoja na mtoto wake.
Hata hivyo amewatolea uvivu wale ambao wanashinikiza afanye vipimo vya DNA kubaina kama kweli mtoto wake huyo ni wa Mulamwah kwa kusema kwamba jambo hilo ni lake na Baby Daddy wake huku akisisitiza kuwa kuachana kwao haihusiani na mtoto wao.
Ikumbukwe Mulamwah ambaye ni baba ya mtoto mmoja kwa sasa na baby mama wake Carol Sonnie waliweka wazi uhusiano wao mwaka wa 2017.