LifeStyle

Bahati Afanyiwa Kipimo cha DNA na Mwanamke Anayedaiwa Kuwa Mama Yake

Bahati Afanyiwa Kipimo cha DNA na Mwanamke Anayedaiwa Kuwa Mama Yake

Msanii nyota wa muziki kutoka Kenya, Bahati, ameweka wazi kuwa amefanyiwa kipimo cha DNA pamoja na mwanamke anayedaiwa kuwa mama yake mzazi.

Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Bahati amesema kuwa zoezi la kipimo hicho tayari limekamilika na sasa wanasubiri majibu yatakayochukua takribani siku 14 kutoka hospitalini.

Msanii huyo amekiri kuwa yupo katika hali ya taharuki akisubiri ukweli kubainika, akijiuliza endapo matokeo yatakuwa chanya ataaanzaje safari mpya ya maisha.

Kwa sasa, macho na masikio ya wengi yapo kwenye majibu ya kipimo hicho ambacho kinaweza kubadilisha kabisa simulizi ya maisha yake. Majibu rasmi yanatarajiwa kutolewa ndani ya wiki mbili zijazo, ambapo ukweli wa suala hilo utawekwa hadharani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *