Rapa wa Kenya Toxic Lyrikali amekanusha kuhusika na vurugu zilizotokea jana katika mtaa wa Donholm, Nairobi zilizodaiwa kuhusishwa na bifu lake linaloendelea na kundi la Buruklyn Boyz.
Kupitia taarifa aliyochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, Toxic Lyrikali amesema kuwa haungi mkono vitendo vya vurugu wala uharibifu wa mali. Amesema kuwa ushindani kati yake na Buruklyn Boyz unapaswa kuamuliwa kupitia muziki pekee, si mapigano ya mitaani.
Aidha, aamewataka mashabiki wake kuwa watulivu na kuepuka kuingizwa katika migogoro inayoweza kuleta madhara.
Kwa sasa, vita ya maneno na diss track kati yake na Buruklyn Boyz inaonekana kuendelea katika majukwaa ya muziki, huku kila upande ukijaribu kuthibitisha ubora wake kisanaa.