Gossip

Bahati Ajizawadia Range Rover Mpya Kusherehekea Miaka 33 ya Kuzaliwa

Bahati Ajizawadia Range Rover Mpya Kusherehekea Miaka 33 ya Kuzaliwa

Staa wa muziki kutoka Kenya, Bahati, amejizawadia gari jipya aina ya Range Rover kama sehemu ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ya miaka 33.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Bahati ameposti picha na ujumbe mzito wa shukrani, akitafakari safari yake ya maisha iliyojaa changamoto na baraka.

Bahati ameeleza kuwa anajivunia kuwa na umri wa miaka 33, akiwa baba na mtu aliyebarikiwa kwa njia nyingi. Msanii huyo alikumbuka alikokulia katika makao ya watoto ya ABC Kenya Children’s Home yaliyoko Mathare Slums, ambako aliota siku moja kufikia mafanikio kama anayoyaishi kwa sasa ikiwemo kuwa baba ya familia ya watoto wanne.

Bahati amehitimisha ujumbe wake kwa kusema kuwa anajiona mwenye baraka nyingi na mwenye furaha kubwa, akimshukuru Mungu kwa kumfikisha hatua hiyo muhimu ya maisha yake.

Hatua ya Bahati kujizawadia Range Rover imepokelewa kwa hisia mseto mitandaoni, huku mashabiki na wadau wa tasnia ya burudani wakimpongeza kwa juhudi, uvumilivu na mafanikio yake, wakimtaja kama mfano wa kuigwa kwa vijana wengi waliokulia katika mazingira magumu lakini wakaendelea kuamini ndoto zao

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *