Entertainment

Bahati akoshwa na wimbo wa Dullah Makabila, “Pita Huku”

Bahati akoshwa na wimbo wa Dullah Makabila, “Pita Huku”

Mwimbaji nyota wa muziki toka Kenya, Bahati ameonyesha kukoshwa na ubunifu alioutumia staa wa Singeli nchini, msanii Dulla Makabila kwenye video ya wimbo wake mpya Pita Huku ulioibua mijadala juu ya mengi kufuatia yaliyo zungumziwa kwenye wimbo huo.

Akiacha koment kwenye video hiyo katika mtandao wa YouTube, ujumbe wa Bahati unasomeka, “Huu ni Ubunifu Kaka Yangu. Hongera kwa Muziki mzuri”.

Mbali na Bahati pia na wengine wengi wameacha komenti zao wakiusifia ubunifu uliofanywa kwenye kazi hiyo.

Wimbo wa “Pita Huku” ambao umetoka Jumatatu ya wiki hii umefanikiwa kupata mapokezi makubwa kutoka kwa wadau mbalimbali wa muziki pamoja na mashabiki kwa ujumla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *